Episode 20

13 1 0
                                    

VUTA N’KUVUTE 20

Inaendelea… 

Bila kupoteza muda wowote, Mtanzi alitwaa rununu na kumtwangia Mariko. Mariko alishangaa ni kwa sababu gani kaalikwa na Mtanzi. Alifikiria tena na tena lakini hakung’amua sababu ya kualikwa kule na Mtanzi. Hata hivyo aliamua kuitikia wito ule ambao bado alikuwa na waiswasi nao. Alifika na kumkuta Mtanzi anamsubiri. Katu alikuwa tayari ashaondoka.

“Karibu. Asante sana kwa kuitikia wito wangu.” Mtanzi alianza.

“Asante.” Mariko alijibu huku akiketi taratibu na moyo ukimwenda kasi kwa woga.

“Nimefurahi sana kwako kufika hapa. Sina shaka tutakayoyajadili yatafaulu.” Mtanzi aliendelea.

“Vile vile nimefurahi kukutana na wewe.” Mariko alijitia bashasha bandia.

Kimya kikajiri huku Mariko akijaribu kukisia kusudi lake Mtanzi la kumwita ofisini mwake. Wakati huohuo macho yake yalitalii mandhari ya ofisi ile. Samani ya thamani ya juu yaliipamba ofisi ile. Pasi na shaka pesa zilizotumika kujenga ofisi ile hazikuwa chache. Aliketi kwenye kiti ambacho wakati wowote ungekufanya kusinzia. Sasa alielewa maana ya ‘uongozi wa sasa umelala kazini.’

Sasa nadhari yake ilianza kulinganua maisha yale ya Mtanzi na yale ya kawaida ya wenyeji wa Takia. Alipofika langoni alifanyiwa msako wa kina kuhakikisha hana silaha yoyote. Akaandamwa hadi alikokwenda. Kamera za siri pia zilikuwa kila mahali. Waliandaliwa chakula cha kifahari na ghali mno. Pia kilifanyiwa ukaguzi kabla kiliwe. Haya yote kwake yalikuwa mageni. Alijaribu kupiga darubini maisha atakayoishi punde tu baada ya kuingia mamlakani.
Itaendelea… 

VUTA N'KUVUTE Opowieści tętniące życiem. Odkryj je teraz