Mwanzo wa sura ya 3
Vuta nkuvute inaendelea….
Mariko Sipondi aliketi sebuleni mwake akitazama runinga yake. Alikwisha kutazama mikutano yote miwili ya hadhara yake Tadi na Mtanzi. Alishusha pumzi na kujiegemeza kwenye kochi. Mawazo yake yakawanda mbali na karibu.Mara mlango wa sebule ulibishwa na ndani akajitosa na kumpata Mariko akiwa bado amezubaa. Alitazama uso uliosawijika wake Mariko. Ghafla aligundua kulikuwa na kitu kilichokuwa kikimtatiza.
“Mbona fikira hizo zote?” Alisaili Katu.
“Ninajaribu kudadisi na kuangalia kwa kina wagombeaji hawa wanayo sera gani muhimu itayaowawezesha kutwaa Kiti hiki cha uongozi cha Takia.” Mariko alijibu.
“Ahaa! Na wewe unawachambua vipi wagombea hawa wote? Kuna uwezwkano wa Mtanzi kutetea wadhifa wake?”
Mariko alisita na kumtazama Katu, kisha akaanza kueleza kwa mazingatio.
“Mimi binafsi ningekuwa wa kuamua basi hafai hata kidogo kupewa miaka mingine mitano ya uongozi. Ahadi alizotoa kwenye kampeni iliyopita aliyatimiza Kama asilimia thelathini tu. ”
“Lakini mimi naona anayo nafasi kubwa ya kushinda. Anapendwa na watu Wengi Sana. ”
“Kupendwa huko kumetufaidi nini ila madhila matupu miaka hiyo yote mitano? Kupenda kusiko faida ni upofu wa hali ya juu. Hayo ndiyo mapenzi yasiyofaidi; mapenzi mapofu.”
Itaendelea…

YOU ARE READING
VUTA N'KUVUTE
Mystery / ThrillerMtanzi ambaye ni Kiongozi wa Takia na mgombea kiti cha uongozi cha Takia anaonyeshwa kama kiongozi aliyejaa udhalimu, majivuno, kiburi, na ukatili. Harakati za kumng'atua uongozini zinaanza Lakini pia wale wanaopania kufanya vile haijulikani Hulka y...