Episode 27

10 1 5
                                    

Inaendelea… 

*   *   *   *

Mtanzi alingojea kwa hamu ofisini mwake Katu na mhazili afike. Alikuwa amezipokea habari za kutoweka kwa Mariko na alikuwa amejawa na furaha ajabu. Sasa alianza kuwaza jinsi aytakavyomshinda Tadi na atakavyozidi kukaa mamlakani kwa muda mrefu. Mara mlango wa ofisi yake ulibishwa na ndani wakaingia Katu na Mhazili. Uso wake Mtanzi ulingaa kwa tabasamu nzito huku akiwakaribisha na kuwaashiria waketi. 

“Kazi ishafanyika?” Mtanzi alisaili kwa hamu. 

“Kazi tumeifanya na imekamilika.” Mhazili alihakiki. 

“Vizuri kabisa. Kilichobaki sasa ni mimi kusalia mamlakani na kuiongoza Takia ninavyotaka. Vizingiti vyote sasa karibu tunavimaliza kuviondoa.” Tadi alizidi kufurahia. Upesi aliingia kwenye shubaka kubwa na kuchomoa mkoba ulikuwa na pesa.

“Huu hapa ni kujitakia wenu kwa kazi nzuri mliofanya. Hakikisha kuwa kila mmoja amepata mgao wake. 

“Ndiyo. Lakini bosi si wajua sisi tutahitaji zaidi? Kazi hii haikuwa rahisi.” Katu aliomba.

“Haha nafahamu hilo kabisa. Umesahau kuwa hivi karibuni tutakuwa tunaogelea kwenye bahari ya pesa? Nitawalipa maradufu.” Mtanzi alihakikisha. 

“Hivi sasa tunafaa kupanga jinsi tutakavyojilinda dhidi ya wapelelezi wowote watakaojaribu kuufichua ukweli juu ya kifo cha Mariko. Natumai kuwa mlihakikisha hamna kitu kitakacho tutia matatani pale mlipoiacha mwili wake. Ingawaje nashangaa hadi sasa polisi hawajapata mwili wake. Polisi wa Takia nap ni vigoigoi sana.” Mtanzi alicheka.

“Hata usiwe na shaka. Tuna uhakika hawatafahamu ukweli na hata wakijaribu kuleta ujuaji si wewe Mtanzi wajua hatima yao?  Najua hawatajaribu.” Katu alijitia ujasiri. 

“Sasa naona ni wakati wangu wa kuondoka.” Mhazili alidai.

“Bila shaka uko huru kuondoka. Ni lazima umechoka kwa kazi hiyo ngumu. Nenda ukapumzike.” Mtanzi alimshukuru Mhazili huku akitabasamu. 

Katu na Mtanzi Pia waliagana Nate Mtanzi akaelekea kukamilisha kampeni zake akiwa na furaha kuu. Kutoweka kwa Mariko haingeweza kuathiri tarehe ya uchaguzi na hivyo wafuasi wa Mariko hakuwa na kingine. Wakabaki kusononeka tu. 

Itaendelea… 

VUTA N'KUVUTE Where stories live. Discover now