Episode 29

7 3 1
                                    

Mhazili hakusema lolote. Alikimya akisikia Mariko akiongea. Ndani kwa ndani alimhurumia ila alijua kuwa kwenda kinyume na matakwa ya Mtanzi ni kujichimbia kaburi. Hatimaye walifika pale aliposema ni pahali salama. Ulikuwa mtaa wa Matambiko. Mtaa uliokuwa nyuma
kimaendeleo mjini Takia. Mariko akatolewa garini na akafungiwa chumba cha kupanga.

"Haya ndiyo makao yako kwa muda kabla yangu kukusafirisha akhera. Hapa hauhitaji kukaa gizani tena." alisema Mhazili. Akaukomelea mlango na akaelekea kwa Mambo kurudisha gari.

Giza lilianza kuingia taratibu. Alifanya hima. Alitaka kupumzika vya kutosha kwani siku
iliyofuata Ilikuwa ni siku ya mwisho ya kuendesha kampeni na alijua Mtanzi angemhitaji.

Wakati huo huo Mariko aliwasha umeme pale chumbani na alishangaa alichokiona. Makochi ya thamani kubwa yaliipamba chumba kile. Chumba chenyewe kilikuwa kimepambwa ungedhani kwa mfalme. Runinga kubwa ilisimama juu ya shubaka kubwa lililochukua takribani upande moja wote wa chumba kile. Mariko alipigwa na kibuhuti asijue la kufikiria. Alikuwa auliwe, Mbona aletwe kwenye chumba chenye thamani kiasi kile? Kilikuwa na kila kitu. Maji, chakula ila hakikuwa na mavazi.

* * * *

Karisa alifika nyumbani kwa Mariko jioni hiyo kabla ya siku iliyofuata ambayo ndiyo ilikuwa

siku ya kuingia debeni. Alimkuta Sumeha na mwanawe wakiwa katika hali ya simanzi kuu

kwani tangu kutoweka kwa Mariko hakukukwa na habari kamili kuhusu kutoweka kwake.

Sumeha alipomwonma Karisa, simanzi yake iligeuka kilio cha kite. Machungu aliyokuwa nayo

moyoni yalikuwa mno. Alikumbuka alipomwonya mumewe kuwa siasa haikuwa mchezo mzuri

na hata akamwambia arudi nyumbani wakaishi kwa raha kama zamani.

Huku ndiko ubepari na ulafi wa kujitakia makuu umetufikisha. Tuko tayari kufanya lolote
kubakia mamlakani hata kama utagharimu maisha ya wazalendo wenye nia njema.” Karisa
alijipata amenena kwani kilio chake Sumeha kilimgusa sana.
Sumeha akafuta machozi kwa kiganja chake na kumtazama karisa. “Hivyo ndivyo kumaanisha
nini?”
“Sina uhakika wala thibitisho ya madai haya lakini hapana shaka kutoweka kwa Mariko ni kwa
sababu za kisiasa. Kuna watu hapa Takia ambao hawataki kutoka uongozini wakijua fika kuwa
wakiondolewa basi na maovu yote waliyotenda yatafichuka. Kila aliye na nia njema ya kuleta
unadhifu wa kisiasa mjini Takia hutendewa unyama wa hali ya juu. Ni mara ngapi watu
waliojitokeza kupinga sera za uongozi tawala huuliwa? Hiki si kisa cha kwanza kutokea hapa
Takia.” Karisa alisema.
“Mimi mwenyewe nilimweleza mume wangu kuwa awe ange sana maana hajui nini
kinachopangwa na mahasimu wake wa kisiasa.” Sumeha aliendelea.
“Hasa. Kinachotendekea viongozi kama Mariko ni thibitisho tosha kuwa Takia na viongozi wake
ni maadui wa nia njema. Na si hilo tu. Upelelezi nao haujazaa matunda tangu kutoweka kwa
Mariko. Hawa wapelelezi wanafanya kazi gani? Mbona wawaache katika mtanziko huu wa
kutojua kilichomfika Mariko?”
“Hatujui tutalia hadi lini. Afadhali tungejua kama yuko hai au maiti. Kila siku tukifika kituo cha
polisi tunachoambiwa ni kuwa uchunguzi bado unaendelea.Hadi lini?” Sumeha aliendelea
kusikitika.
“Hapa Takia twaishi kwa maridhia ya mola. Wacha tumwombe kuwa ataturehemu toka
mikononi mwa mabeberu hawa.

VUTA N'KUVUTE Where stories live. Discover now