Episode 31

3 2 0
                                    

“Aa-ah! Samahani. Wajua wakati mwingine fikira hutukosesha usingizi.” Mhazili alijitetea.

“Fikira zipi wakati maisha yanatuendea shwari? Yule duduvule aliyekuwa anatuwanga kichwa
sasa naamini anaendelea kuoza na kuozeana popote alipo. Mbona uwe na fikira na hivi karibuni
tutakuwa tunaishi raha mustarehe?” Mtanzi alitanua kifua.

“Hasaa. Hilo nalifahamu bayana.” Mhazili alicheka kicheko kifupi. "Bwana Masumbufu yu wapi?”

“Atatukuta shuleni Bahati. Natumai yuko njiani kwa sasa.” Mtanzi alihakiki.

“Lakini mbona ukamchagua Matata awe naibu wako wakati historia yake kama kiongozi si nzuri?
Huoni kuwapo kwake huenda ukakukosesha kura? Watu huenda wakaona wanafiki wawili
wameungana wakatae kukupigia kura.”

“Hahaha!” Mtanzi hakujizuia kuangua kicheko. "Alikwambia nani kuwa nategemea kura zao
kupata ushindi? Haijakuwa hivyo rafiki yangu. Kunazo mbinu mbadala za kuhakikisha tunabaki
mamlakani liwalo na liwe."

“Ahaa kumbe! Hivi mbona siri hii hujawahi kuniambia?” mhazili alisaili.

“Kwa sababu siri hii ni ya wachache wetu. Wale wanaoambiwa siri hii hawaishi muda mrefu.” Mtanzi alisema.

Lo! Mhazili hakuamini masikio yake. Mara waling’oa nanga kuelekea shuleni Bahati baada ya kuhakiki kuwa Tadi na wafuasi wake wameondoka. Mtanzi akafungua juu ya gari lake na kuanza kuwaongelesha wafuasi wake. “Pesa kwenu kura kwangu!”

“Ndiyooo!” umati uliitikia huku waking'ang'ania vijinoti vilivyokuwa vikirushwa hewani naye
Mtanzi. Alirusha noti nyingi huku wanatakia walalahoi wakiziparamia kwa pupa angalau wazinyake kabla hazijafika chini. Aliyekuwa mnyonge hakuwa na bahati maana ilikuwa mwenye nguvu mpishe. Alivyozidi kuzirusha noti zile ndivyo umati ulivyozidi kuongezeka.

Hatimaye walitua shuleni Bahati kwa kishindo. Kila mmoja akapiga kura yake. Hata hivyo Mtanzi hakumwona Mhazili katika foleni ile ya kura. Kumbe alikuwa amebaki garini.

VUTA N'KUVUTE Where stories live. Discover now