Episode 32

4 1 0
                                    

* *
        Mariko aliangaza macho yake pale ndani na kushangaa nia ya yule aliyemleta pale ilikuwa gani. Alikuwa hapo awali amesikia kuwa shughuli za kumtafuta zilikuwa zimesitishwa hadi kukamilika kwa uchaguzi. Punde fikira ilimjia. Alifungua runinga ile iliyokuwa pale ndani kutazama nini kilichokuwa kikijiri. Machozi yalimlengalenga kwa ghafla alipoona umati jinsi ulivyojitokeza kuchagua kiongozi wa mji wa Takia. Ghafla picha zilimwonyesha Mtanzi akihutubu baada ya kupiga kura yake na kuelezea matumaini yake ya kuibuka mshindi.

“Ninayo furaha siku ya leo kuwa mmoja kati wagombea wa kiti hiki cha kuuongoza mji huu wetu.
Natumai kuwa mumeona maendeleo ambayo tumefanya katika miaka mitano iliyopita na natumai mtatupa nafasi nyingine ya kuitimiza ruwaza ya mji huu. Ni wazi kuwa uchaguzi
tutashinda na nawahakikishia wapinzani wetu, ikiwa hawatashinda, kuwa tuko radhi kufanya kazi nao.
Mimi nikichaguliwa nitahakikisha kuwa mji huu unaendelea mbele…!”

Mariko aliizima runinga
ile maana hakutaka tena kusikia zaidi uwongo wake Mtanzi. Alijipweteka kochini kwa kilio cha kwikwi. Kilio ambacho hakikuwa tu cha kukililia hali yake ya sasa ila kuwalilia wanatakia ambao walikuwa wakiikodolea macho dhulma ijayo bila mtu yeyote wa kuwaauni.

Alisogea mlango na kuujaribu lakini ulikuwa umekomelewa komekome. Alikosa subira na vilevile kuhisi moyo wake ni mzito. Aliyaona maisha yake hayana maana tena. Hata kama jamaa yule hangemuua bado angeishi tu katika dhulma ya uongozi wa Takia na hivyo ndivyo hali itakuwa kwa miaka mitano ijayo. Sasa aliomba Tadi angalu ashinde uchaguzi ile. Si kwa sababu Tadi alikuwa afadhali bali alikuwa labda 'nusu shari'.

Kwa upande mwingine Tadi hakuwahi kuwa kiongozi wa Takia na hivyo alidhamiria huenda mambo yakawa afadhali kidogo chini ya uongozi wake. Hata hivyo alijua kuwa kwa Tadi kushinda ni kama
kwake kuukwea mchongoma.

Pale ndani hakuona maana ya kuishi tena. Alifikiria kuongozwa na Mtanzi na Masumbufu na kuona ni heri kufa. Alifikiria juu ya kujitoa uhai. Macho yake yakatua kwenye upanga uliokuwa umetundikwa ukutani. Kwa mwendo wa kunyatia, akaufikia upanga ule na kuuuchomoa. Akasimama pale kwa sekunde kadhaa na machozi ya kite yakafurika machoni mwake.

VUTA N'KUVUTE Où les histoires vivent. Découvrez maintenant