Episode 10

18 3 0
                                    


Inaendelea… 

Katu tangu waagane na Mariko alijawa na mawazo mengi sana. Alikuwa ni mfuasi sugu wake Mtanzi na alionekana kumtetea kisirisiri. Hata hivyo hakuwa na ujasiri wa kumsifia mbele ya Karisa au mtu yeyote yule aliyekuwa mgeni kwake. 

Urafiki baina ya Katu na Karisa haukuwa ule tu wa kawaida. Kando na kuwa rafikiye Karisa alikuwa msiri mkubwa wake Mtanzi. Hata hivyo Karisa hakufahamu hilo. Haikuwa imemjia mawazoni kuwa Katu alikuwa katika harakati za kubadilisha mtazamo wake wa kisiasa. 

Alikumbuka bayana siku moja alipoitwa na Mtanzi ofisini mwake. Alishangaa ni mkutano upi au ni dharura ipi aliyekuwa nayo Mtanzi. Basi alijitosa ndani ya gari lake aina ya Lamborghini alilopewa na Mtanzi licha ya kudai mtaani kuwa alilinunua kwa jasho lake.

Alifika ofisini na kumkuta Mtanzi tayari anamsubiri. Wakaamkuana kwa bashasha huku Katu akiketi mbele yake Mtanzi. 

“Naam! Habari za siku nyingi?” Mtanzi alianza. 

“Salama kabisa.” aliitikia Katu. Akatikisa kichwa huku akimtazama Mtanzi. 

“Nina kazi yako.” 

“Kazi? Ya aina gani?!”

“Kazi rahisi sana. Naelewa kuwa nyama yako ya ulimi ni tamu sana. Hivi kazi hii haitakushinda. Alisimulia Mtanzi. 

“Ahaa!  Kabisa. Nikirusha chambo pasi na shaka huwa ninanasa.” Katu alijishaua. 

Itaendelea… 

VUTA N'KUVUTE Où les histoires vivent. Découvrez maintenant