Episode 9

22 3 0
                                    

 Inaendelea… 

Watu wengi waliyakumbuka na kuyakariri kwa kina maneno ya hotuba yake ya kwanza;

“Najua mnashangaa kaibukia wapi jamaa huyu. Ni masikitiko makuu kuona jinsi wanasiasa wanaotarajiwa kuitwa waheshimiwa wakifanya sarakasi na vitimbi hadharani. Badala ya kuuza sera zao kwa umma hawaishi kushutumiana, kupigana vijembe na kutusiana hadharani. Watawapa pesa ili kuwashawishi muwaone wazuri. Ahadi wanazotoa ni zile za kutufumba macho tusione ufidhuli na ukatili ulioko ndani yao. Kibarua chao kikuu mamlakani ni kujipa kipaumbele badala ya kuipa mji huu kipaumbele. Hawana tofauti na uzuri wa mkakasi ambao ndani yake ni kipande cha mti. 

“Wenzangu tusiwe Kama wapita daraja iliyoundwa kwa miti, ambayo licha ya miti ile kuoza na kutishia kututumbukiza ndani ya mto, tutazidi tu kuvuka bila kujali. Mbona tusitafute miti mipya ama tujenge daraja la saruji? 

“Si ajabu kuona umaskini ukitukaba kila uchao kwa kukosa mahitaji ya kimsingi. Mifumko ya bei za bidhaa muhimu, ubovu wa miundo msingi kati  ya uozo nyingine nyingi ni baadhi tu ya madhila yanayotukumba. Nawaulizeni,  Mbona tufe kwa ndwele wakati tunazo tembe za kujitibu?”

Inaendelea… 

VUTA N'KUVUTE Donde viven las historias. Descúbrelo ahora