Episode 7

19 3 0
                                    

Inaendelea….

“Hahaha!” Sumeha hakuweza kujizuia kuangua kicheko. “Acha utani yakhe.”

“Aka! Huu si utani. Kuna utani mwingine mkuu kuliko huu?!” Aliuliza Mariko akiinyooshea kidole runinga yake. Sumeha na Katu wakabaki kutumbulia macho runinga Kama kwamba ilikuwa na jibu la swali lake Mariko. 

“Mariko mume wangu, wajua kuwa huna pesa za kuendesha kampeni. Pia umaarufu hauna. Nani  atakayekutambua mji huu wa Takia isipokuwa mimi mkeo na wanao? Chama gani maarufu utakachotumia? Huoni azma hii yako ni Kama ndoto isiyojulikana Kama itawahi kuwa kweli? ” Sumeha alinadi kwa mumewe. 

Mariko aliinuka ghafla na kumkita mkewe jicho kali na kisha kuketi taratibu huku akisema;

“Siasa si pesa, si umaarufu wala si chama. Pesa hizo unazosema ni za nini?  Kuwahonga watu kusudi wakupe kura zao? Umaarufu hauna faida ikiwa umaarufu wenyewe utatumiwa kunyanyasa watu. Chama nacho  ni gari tu. Na gari bila barabara ni gari tu,  haikufikishi popote. Ikiwa tutaendelea kuangalia au kuchagua viongozi kulingana na Chama umaarufu au hata pesa pasipo kuzingatia sera, basi tofauti yetu na nazi mbovu ni ipi?” Mariko alitoa dukuduku lake. 

“Mmmmmh!” Katu alisafisha koo. “Mariko,  waelewa kuwa siasa za mji huu huwa na imebaki kuwa hivyo tangia mkoloni kuonyeshwa mlango. Unadhani nani atakusikia?”

“Hasaa! Alidakia Sumeha. “Wananchi wenyewe hawawezi kukusikia. Wajua kuwa siasa zetu pasi na pesa huwezi. Siasa zetu pasi na umaarufu hutoweza. Fauka ya hayo, Kama chama unachokitumia hakijulikani  haupati chochote. Kura hupigwa kwa mazingatio hayo.”
Itaendelea…..

VUTA N'KUVUTE Where stories live. Discover now