Inaendelea…
“Uwoga wenu unanitia machungu. Mbona mgonjwa akubali kufa wakati anayo uwezo wa kupata matibabu? Ndiyo hali yetu hii. Tumekubali viongozi kufanya watakavyo. Mbona isije siku moja wanamji wa Takia watasimama na kukataa uongozi uliojaa usodai? Najua kuna wengi walio na maono Kama yangu lakini uwoga umewafanya wasitoe sauti.” Mariko alitongoa.
“Basi kila la mwenzi wangu.” Katu alishusha pumzi. “Lakini kumbuka siasa za mji huu ni Kama kujitupa ndani ya bahari ya kina kirefu. Vitu vitatu ndivyo vinavyoamua hatima yako. Ukiwa navyo utapita, pasi nacho utaanguka.” Alisema akiondoka.
Sumeha alibaki katika hali ya taharuki. Moyoni alitamani mumewe aghairi nia yake. Aliomba usiku na mchana lakini Mariko aliazimia ima fa ima, liwalo na liwe, kuwa angeirejesha imani ya wanatakia. Aliomba pia mumewe asije akaambukizwa ‘ugonjwa wa wanasiasa’. Alikuwa amewaona wengi waliokuwa Kama Mariko mwanzoni na punde tu baada ya kuingia mamlakani, wakavua ngozi ya kondoo na kuonyesha kuwa wao ni chui halisia.
Bwana Mariko Sipondi, sasa mwanasiasa , alikamilisha matakwa yote ya tume ya uchaguzi na kampeni akaanza rasmi. Ilikuwa vigumu kwake kuanza lakini uchu wake haukumpa kurudi nyuma. Ulikuwa ni uamuzi ulioamuliwa kwa moyo moja. Wengi waliosikia habari hizi walipatwa na mshangao mkubwa. Wakadhani ni mzaha lakini wakajua ukweli Mariko alipoanza kampeni rasmi.
Itaendelea….
ESTÁS LEYENDO
VUTA N'KUVUTE
Misterio / SuspensoMtanzi ambaye ni Kiongozi wa Takia na mgombea kiti cha uongozi cha Takia anaonyeshwa kama kiongozi aliyejaa udhalimu, majivuno, kiburi, na ukatili. Harakati za kumng'atua uongozini zinaanza Lakini pia wale wanaopania kufanya vile haijulikani Hulka y...