VUTA N’KUVUTE 11
Inaendelea…
Mtanzi akitabasamu akisema,”basi si wajua mji huu Wetu una watu wachache ambao hujifanya wangwana na wastaarabika? Wanadai wachangnuzi wa kukagua na kuchanganua wakati kazi yao ni kuchochea umma dhidi ya uongozi wetu.”
“Naam!” aliitikia Katu.
“Watu Kama hao wanafaa huwekwa panapowafaa.” aliendelea Mtanzi. “Wanajifanya vipofu wasioona mengi mazuri tuliowatendea wanatakia.”
“Sasa kazi ni gani mwenzangu?”
“Si wamfahamu huyu Karisa?”
“Vizuri sana.”
“Huyo sasa kazi yako kumnyamazisha na kumkumbusha yale yanayowapata wale ambao hujaribu kuchimbua mishipa yetu ya uhai. Si wajua kunadi vizuri? Basi jaribu kumshawishi kwa vyovyote vile atuunge mkono.”
“Sawasawa mkubwa. Kazi ntaifanya tena kwa bidii.”
“Bidii yako utajiri wako.” Mtanzi alinena akiangua kicheko kikubwa cha kejeli.
Happy Kati aligutuka toka mawazoni na kujaribu kufikiria hatua alizopiga katika kazi hii aliyopewa. Hakuona maendeleo yoyote. Karisa ni Kama alizaliwa na msimamamo wake. Hakuweza kuwewesuka hata kidogo. Akiwa bado anapiga bongo, Karisa alijitosa ndani ya sebule yake. Baada ya kujuliana hali, Karisa alimuanza.
“Waonekana mwenye fikira kweli. Nini kinachokupitikia akilini?”
“Mmmmh!” aliguna Katu huku alishusha pumzi.” Si chama mno hasa. Maisha haya wakati mwingine hushughulisha akili zetu.”
“Ahaa! Ndivyo.” kimya kikajiri kidogo. “Wewe umesikia habari hii iliyo hewani?” Karisa aliuliza.
“Habari gani hizo?” Katu alimakinika.
Itaendelea…
YOU ARE READING
VUTA N'KUVUTE
Mystery / ThrillerMtanzi ambaye ni Kiongozi wa Takia na mgombea kiti cha uongozi cha Takia anaonyeshwa kama kiongozi aliyejaa udhalimu, majivuno, kiburi, na ukatili. Harakati za kumng'atua uongozini zinaanza Lakini pia wale wanaopania kufanya vile haijulikani Hulka y...