Episode 6

21 4 0
                                    

 Inaendelea….

Hatufai tena kupiga kura kwa ‘mtu wetu’ au tunayempenda. Uongozi si maumbile, si mapenzi, si chama ila ni mwito. Uongozi ni maono na mwongozo wa kuweza kutumikia watu. Kuboresha maisha ya watu. 

Katu alibaki kutikisa kichwa. Mariko naye aliendelea kumwongelesha katu.  Jazba sasa ilianza kumpanda. 

“Badala ya wanasiasa kushindana kwa sera na jinsi ya kuboresha maisha yetu, wanapuliza tu tarumbeta za propaganda zisizowafaidi wananchi kwa vyovyote vile. Kazi yao kubwa ni kushutumiana na kuhonga watu hadharani.  Ni mara ngapi wametoa ahadi ambazo kuzitimiza kumekuwa muhali?”

Katu alimkodolea macho Mariko Sipondi. Hakujua ni kitu kipi kilimchochea kiasi cha kutiririkwa na maneno kiasi kile. Pasi na shaka alizungumza kama mwanasiasa aalimu. Mtu aliyeona udumakuwili ndani na nje ya matamshi ya wanasiasa. “Ama kaazimia kujitosa siasani? ” Katu alihofia kimoyomoyo. Wakati huu wote kimya kilikuwa kimetawala baina yao. 

“Nitaingia katika siasa!” Mariko alisema ghafla. Hili lilimpata katu Kama dhoruba kali. Alichanganyikiwa kiasi, akainuka na kwenye kochi na kuketi tena. 

“Wa-wasema nini?!” Katu aligugumiza. 

“Nitaingia siasani.  Hali si hali ikiwa viongozi tunaotarajia kutuongoza wataendelea na tabia hizi zao hasi. Penye nia pana njia.” 

Mara mlango ulifunguka na ndani akaingia Sumeha,  mkewe Mariko. Alikuta mtanziko ukiwa umewagubika Katu na Mariko.

“Wahaka ni ya nini?” aliuliza Sumeha kwa hamu. 

“Akwambie mwenyewe Mariko!” Katu alinena. Sumeha akamgeukia mumewe kwa mtazamo wa wahaka na matumaini pia.

“Nimeamua kuwa kinyanganyiro hiki cha ikulu lazima nijitose ndani!” alirudia Mariko.
Itaendelea……

VUTA N'KUVUTE Where stories live. Discover now