Episode 26

8 1 0
                                    

VUTA N’KUVUTE 26

Inaendelea… 

Alingoja akangoja hatimaye akachoka. Akaamua kulala ila usingizi ulimwambaa, hakupata hata lepe. Simu yake ilipokereza alitoka shoti kuitazama kwa matumaini kuwa pengine angekuwa ni mumewe. Wahaka ulimjaa na kumtawala. Mbona Mariko hajampigia kumweleza sababu ya kuchelewa kwake? Mbona simu yake imezimwa? 

Siku iliyofuata baada ya kungoja bila kuona dalili za kurejea kwa mumewe, Sumeha aliamua kupiga ripoti kwa polisi. Habari za kutoweka kwa Mariko Sipondi zikaenea kwa kasi mji wote wa Takia. Kuna wale waliopatwa na mshangao kupokea habari zile. Kuna wale waliosikitikia Sana kutoweka kwa Mariko sababu ya imani waliokuwa nayo kwake. Kuna wale hawakuamini Kama katoweka tu ila walijua kuna mengi yaliyojisitiri ndani ya neno ‘katoweka’. Kuna wengine waliofurahia kutoweka huko kwa Mariko. Ilimradi kulikuwa na hisia mseto kuhusu kupotea kwa mwanasiasa changa zaidi mjini Takia. 

Haikuwa mara ya kwanza kwa mtu mwenye maono yanayokinzana na walio uongozini kutoweka kiajabuajabu. Cha kushtua zaidi ni kuwa baada ya mtu kutoweka aghalabu hupatikana akiwa maiti. Wazo hili lilimjia Karisa na akajua fika kuwa kupotea kwa Mariko Sipondi Haikuwa kisa  cha kubuni ila ni mpango wa kuendelea kuizima ndoto ya kuikomboa Takia kutoka kwa mwafrika mkoloni. Hiki kilikuwa ni kisa kingine cha wanatakia kupokwa haki, kunyimwa usemi na kuchezewa kayaya za chini kwa chini.

Itaendelea… 

VUTA N'KUVUTE Onde histórias criam vida. Descubra agora