Episode 15

11 2 0
                                    


Inaendelea… 

“Nani huyo?” Sumeha alitaka kujua. 

Mariko akaashiria runinga. Sumeha hakuamini alipoona kilichojiri. Kichwa cha habari kilisoma, ‘WAFUASI WA MARIKO NA TADI WAKABILIANA.’ sumeha hakuamini macho na Masikio yake. Machozi yalianza kumtoka njia mbilimbili. 

“Ghairi nia mpenzi. Wangekupata wewe vijana hawa ni yepi yangetokea? Huu ni mchezo mbaya. Rudi nyumbani tukaishi kwa furaha kama hapo awali. Siasa haileti raha ila hofu tupu.”

*   *   *

Hata hivyo baada ya kuondoka kutoka mkutano ule, Tadi Makumbo alipoteza fahamu. Kikichomshtua ni kuona watu wengi sana wakimshangilia Mariko kuliko yeye. Hii ilimshtua na akazirai. Alikuwa mzee sana. Tadi alikimbishwa hospitali  mara moja na kulazwa.

Mkewe Bi. Mterehemezi alikaa kando yake akimhirumia mumewe  kwa msiba ule. Hali hii ilimkumbusha zamani sana kabla ya kuaga dunia kwa babake. 

Sauti,  Kama alivyoitwa babake,  alikuwa amekumbana na migogoro iliyohusu Shamba lao. Migogoro hiyo ilianza kuchipuka tu hivi maajuzi baada ya kufichika kwa miaka mingi. Ilibainika kwamba shamba lenyewe lilikuwa limenyakuliwa zamani punde tu baada ya  mji huo kujipatia uhuru. Akiwa na uchu ya kuwekeza na kutengeza pesa, Sauti alilinunua ardhi yenyewe toka kwa mwanasiasa moja aliyekuwa ushawishi mkubwa. Akajenga kiwanda kikubwa ambacho alikienzi Sana. Alipata faida kubwa kutokana na bidhaa za kiwanda hicho. Sauti akatajirika pakubwa. Akawasomesha wanawe hadi upeo wa juu. Hivyo aliukumbatia bahati ya kuwa na kiwanda kile kwa dhati  ya moyo. 
Itaendelea… 

VUTA N'KUVUTE Hikayelerin yaşadığı yer. Şimdi keşfedin