Episode 14

17 2 0
                                    

VUTA N’KUVUTE 14

Inaendelea… 

“Hamjafanya jambo la busara.” alianza Mariko. “Kila kiongozi anayo haki ya kusikizwa bila kuleta mifarakano yoyote. Mimi hapa sijakuja kuzua zogo wala kuvuruga mkutano wa mtu. Nilikuja kumsikiza Tadi. Sisi wagombeaji hatufai kuwa maadui bali marafiki.”

Mariko alishuka toka jukwaani na kuelekea nyumbani kwake. Hata Kabla hajaenda Sana, alisikia mayowe kutoka uwanja wa Tuungane. 

Alipofika kujionea nini kilichokuwa chanzo cha mayowe yale, alipatwa na kihoro kuona watu wengi wamejeruhiwa vibaya na vijana ambao sasa walikuwa wamepanda lori kubwa tayari kuondoka. 

Walikuwa wakiimba jina lake Tadi. Lo! Mariko hakuamini macho na masikio yake. 

Bila kupoteza muda wowote Mariko alipiga ripoti kwa polisi. Manusura wakakimbizwa hospitali ya rufaa ya Tuungane. Hata hivyo, watu kumi na sita waliangamia katika makabiliano yale. Mariko alitazama kwa huruma, Kilio kikiwa kimehanikiza hewa. Hakujua kuwa azma yake ya kutaka kuiongoza Takia ingegharimu maisha ya wanatakia. Hakuweza kujisamehe kwa tukio hilo. 

Alifika nyumbani na kumkuta mkewe anatayarisha chajio. Sumeha kumwona tu mumewe aligundua kuwa kuna kitu kilichokuwa kikimtatiza. 

“Nilikwambia Siasa ni mchezo mbaya. Siku ngapi utaishi ukiwa umenuna kiasi hiki?” Sumeha alimwaga dukuduku lake. 

“Sifahamu watu wengine waliuzika wapi utu. Mbona mtu akubali kulipwa kusababisha kifo  cha mwenziye?” Mariko alisaili kwa masikitiko makuu. 
Itaendelea… 

VUTA N'KUVUTE Where stories live. Discover now