Episode 13

17 2 0
                                    

VUTA N’KUVUTE 13

Inaendelea… 

*   *   *

Wakati huohuo, Tadi Makumbo wakiwa na Fahama Makumbo waliendelea na kampeni zao. 

Mkutano huo uliandaliwa katika uwanja mdogo wa shule ya Bahati katika eneo la Tuungane. Tuungane ulikuwa ni mtaa aliyoishi Mariko Sipondi na familia yake. 

“Msije mkadanganywa na wanasiasa wengine ambao nia yao ni kujitakia makuu.” Tadi alipaaza sauti. “Wanadai kuwa na uwezo ilhali ni maneno matupu.” aliendelea kutia pondo. Mariko alikuwa miongoni mwa hadhira yake Tadi. Alikuwa amejibanza katikati ya umati ule kumsikiza Tadi. Tadi mwenyewe hakuwa na habari yoyote kumhusu Mariko bali Tuungane yote ilimjua na kumfahamu Mariko. 

“Mimi ndiye mkombozi wa mji huu. Nimefahamu fika azma ya wapigianaji uhuru wetu na ninayo hakika  mkinipa kura ntawafikisha walikonuia waanzilishi wa mji huu.”

Ghafla, umati uliokuwa umeketi pale nyuma ulianza kupaaza sauti huku wakiliimba jina lake Mariko. Wakambeba juu juu huku wakiimba na kumsifia. Tadi alisitisha hotuba yake ghafla na umati wote ukageuka kutazama nyuma. Tadi alipigwa na bumbuwazi asijue kilichokuwa kikiendelea. Licha ya juhudi zake Mariko kutuliza mihemko ya umati ule, hawakusita kumshangilia. 

Tadi alitazama wandani wake, kisha akamwashiria Fahama Makumbo waondoke. Wakaingia garini na kuondoka. Mkutano wake uligeuka ghafla na kuwa wa Mariko. Barobaro wakambeba Mariko had jukwaani na kumtaka ahutubu. 

Itaendelea… 

VUTA N'KUVUTE Hikayelerin yaşadığı yer. Şimdi keşfedin