Inaendelea…
Siku moja alipokea ujumbe wa simu. Ilisoma hivi:
“Twakupea ilani ya siku tatu kuondoa kiwanda chako hapo shambani maana shamba lenyewe si lako. Kinyume na hayo, tutakuondoa kwa nguvu.”
Ujumbe huu uliacha fundo chungu moyoni mwa Sauti. Akazirai. Kuzirai huko ndiko kulimfanya kuipungia dunia mkono wa buriani. Siku tatu baadaye kiwanda chake Sauti kilitwaliwa na shamba lake kunyakuliwa. Juhudi za mamake Mterehemezi kutafuta haki makortini hazikufua dafu kwani kila mara kesi yao ilitupiliwa mbali kwa madai ya kukosa ushahidi tosha.
Yalikuwa ni masaibu yaliyoikumba aila yake Sauti. Familia iliyojaa faraja ikabaki hohehahe kwa simanzi tele. Hata hivyo mola hamwachi mja wake. Mterehemezi alisomeshwa na wahisani hadi alipomaliza chuo kikuu. Alifuzu vizuri kwa daraja ya kwanza na hivyo muda mfupi baadaye aliajiriwa Kama mhasibu mkuu katika benki kuu ya mji wa Takia.
Itaendelea…
YOU ARE READING
VUTA N'KUVUTE
Mystery / ThrillerMtanzi ambaye ni Kiongozi wa Takia na mgombea kiti cha uongozi cha Takia anaonyeshwa kama kiongozi aliyejaa udhalimu, majivuno, kiburi, na ukatili. Harakati za kumng'atua uongozini zinaanza Lakini pia wale wanaopania kufanya vile haijulikani Hulka y...