Episode 36

13 0 0
                                    

SURA YA SITA
Baada ya kuchaguliwa kwa Mtanzi na Matata, Inspekta Hatmi aliamuru uchunguzi kuendelea kubaini kilichopelekea kifo chake Mariko. Hatmi aliongoza operesheni hiyo kubwa na ngumu ila alijua fika kuwa kama Mtanzi alihusika basi hakuna jinsi haki ingewahi kupatikana.

Ghafla walipita vichochoroni na kupata kipande cha kijikaratasi na nguo zilizokuwa zimetupwa kando
ya Barabara. Waliziokota zile nguo na walipofungua, wakaona kuwa zilikuwa zimelowa damu na ndani  ya kijikaratasi kile kulikuwa na maandishi yaliyokuwa yameandikwa kwa kalamu ya mate. Inspekta Hatmi alitwaa kijikaratasi kile na kuanza kusoma maandishi yale kwa sauti:

Kwa wapendwa wangu,
Msijisumbue kunitafuta miye maana nishatangulia mbele yake haki. Ninahisi uchungu
ninapoandika Lakini uamuzi wangu ndio ulioniua. Laiti ningalisikia ushauri wenu nakama
hii haingenifika. Tutaungana tena wakati wenu wa kuabiri basi hili likifika. Inshallah!
Wenu mpendwa
Mariko Sipondi.

Alitazama tena maandishi yale kwa mshangao na kuikunja kijikaratasi kile na kukitia mfukoni. Wote wakaandamana hadi kituo cha polisi. Hatmi akampigia simu Sumeha na kumtaka kufika kituoni mara moja. Sumeha alifika akitumai atapata habari njema kumhusu mumewe.

"Asante kwa kufika." Hatmi alimshukuru Sumeha huku akamwashiria aketi.

"Asante." Sumeha alijibu kwa heshima na kuketi kwa wasiwasi mkubwa.

Nyumbani alikuwa
amemwacha mwanao ambaye hakuwa amerudi shuleni kwa sababu walipewa likizo kidogo kwa
sababu ya uchaguzi. Hata hivyo alihisi upweke mkubwa moyoni kwani kupotea kwa mumewe
ulikuwa kama msumari moto kwenye kidonda. Majukumu yote ya kifamilia sasa yalimwia vigumu. Hapo ndipo alipotanabahi ukubwa wa mwanya aliokuwa ameuacha mumewe pale
nyumbani. Moyo wake ulibaki kulemewa na simanzi kila wakati.

A

lijiweka sawasawa pale kitini angali anamtazama Inspekta Hatmi ambaye alikuwa akifikiria namna ya kumwanzishia. Sumeha naye macho yalionekana mekundu kwa kilio cha kila mara. Kufahamu kufariki kwa mumewe kulimtia majonzi na soni kuu.

"Mimi siamini kuwa Mariko aliliwa tu na wanyamapori. Kwani huyu fisi au simba aliyemla
hakuacha hata vipande vya nyama au mifupa pale alipomlia? Uchunguzi wa kina unafaa kufanywa kubaini ukweli wenyewe." Sumeha alitiririkwa na maneno.

"Lakini kesi yenyewe imekwisha fungwa na hakuna namna ya kuianzisha tena." Hatmi alijibu.

"Ndiyo lakini hatujapata haki na ukweli. Katu siamini kuwa mume wangu aliliwa na mnyama. Damu pekee si thibitisho tosha kuwa aliuliwa na wanyamapori." Sumeha aliyasema hayo na kuondoka ofisini mwake Hatmi kwa kilio cha kwikwi.

* * * *

VUTA N'KUVUTE Where stories live. Discover now