VUTA N’KUVUTE
Inaendelea…
“Ala! Hujasikia habari za mgombea mwingine mpya aliyejitosa siasani juzi?” Karisa alisaili.
“Ahaa kumbe! Nimefahamu sasa. Wamzumgumzia Mariko Sipondi.”
“Ndiyo!”
“Hata hivyo nashangazwa na uamuzi wake huo.” Katu alisema.
“Washangazwa kwa nini?” Karisa alisaili.
“Namfahamu fika Mariko. Huu uamuzi wake ni uchaa tu. Wasemao husema kitanda usichokilalia hujui kunguni wake.” Katu alieleza.
“Naweza nikakubaliana nawe kwa upande moja na nikatofautiana nawe kwa upande mwingine.” Alinena Karisa. “Nakubaliana nawe kuwa huyu ndugu ni mgeni katika uwanda huu lakini tusisahau kuwa hamna yeyote aliyezaliwa akiwa mwanasiasa.”
“Kunao mwenzangu.” Alikaulisha Katu. “Mtazame Mtanzi. Babu yake alikuwa kiongozi, akaja babake na sasa yeye yu mamlakani. Huyu ni kiongozi aliyezaliwa siasani, akalelewa na wanasiasa. Damu ya uongozi inatiririka ndani ya mishipa yake.”
“Ndiyo maana kuna haja ya kuleta mabadiliko. Urithi huu wa uongozi umetufaidi nini? Ukoloni mamboleo na maovu mengine mengi yanazidi kukithiri badala ya kudidimia.” Karisa alipinga.
Katu alijiweka Sawasawa kochini na kumkita jicho Karisa.
“Mimi naona watu wa mji huu wanapenda kuona mabaya tu bila kuona mazuri. Hawaoni mazuri yaliyoletwa na uongozi huu.” Katu alijaribu kutetea.
“Mazuri yapo hatukatai. Lakini ukijaribu kulinganisha mazuri na mabaya, mabaya ndiyo mengi. Ukosefu wa usalama, madeni na kadhalika.” Karisa alifafanua kwa nususi. Katu alibaki kamtumbulia macho. Hakumweza kabisa Karisa.
Itaendelea…
YOU ARE READING
VUTA N'KUVUTE
Mystery / ThrillerMtanzi ambaye ni Kiongozi wa Takia na mgombea kiti cha uongozi cha Takia anaonyeshwa kama kiongozi aliyejaa udhalimu, majivuno, kiburi, na ukatili. Harakati za kumng'atua uongozini zinaanza Lakini pia wale wanaopania kufanya vile haijulikani Hulka y...