Inaendelea…
SURA YA TANO
Katu alifika ofisini kwa Mtanzi kama alivyoitwa. Mtanzi alitaka ripoti yake kuhusu kazi aliyokuwa amempa na pia alitaka kumkabidhi kazi nyingine. Alifika na kumkuta akijiandaa kuendesha kampeni za mwishomwisho kabla ya kuandaliwa kwa uchaguzi mkuu.
“Ahaa! Wasema Mariko Sipondi. Huyo ni jirani yangu hasa. Ni mwenyeji wa Tuungane. Ana mke na mwana mmoja aliye kidato cha tatu katika shule ya upili ya Bahati.” katu alieleza.
“Ni tajiri au ni mtu wa kadri kifedha?” Mtanzi alisaili.
“Si tajiri si maskini ila ni wa kadri hapo. Naamini alichukua mkopo kuendesha kampeni zake. Nashangaa sana anavyopata wafuasi wengi kwa muda mchache. Niliona kama hataweza lakini sasa naona maono yake yana mnato mkuu. Unao mpango gani sasa maana naona ana nguvu jamaa huyu.”
Mtanzi alionekana akiwaza. Akaranda huku na kule kabla kutabasamu ghafla.
“Waonaje tukimweleza atuunge mkono? Tuunde mrengo dhabiti wa kisiasa utakaotuhakikishia ushindi uchaguzini?”
“Kabisa!” alishangilia katu. Hilo ni wazo zuri. “Kisha wale wafuasi wake wote waje upande wako.”
“Ndio.” Mtanzi aliitikia.
“Halafu Tadi hatakuwa na lingine ila kuanguka kama kawaida yake. Hachoki mzee yule.”
Itaendelea…
YOU ARE READING
VUTA N'KUVUTE
Mystery / ThrillerMtanzi ambaye ni Kiongozi wa Takia na mgombea kiti cha uongozi cha Takia anaonyeshwa kama kiongozi aliyejaa udhalimu, majivuno, kiburi, na ukatili. Harakati za kumng'atua uongozini zinaanza Lakini pia wale wanaopania kufanya vile haijulikani Hulka y...